SOKA-SEVILLA-MAN UNITED-MCHEZO

Soka: Sevilla FC yawalambisha Manchester United 2-1

Bruno Fernandes kiungo wa Manchester United.
Bruno Fernandes kiungo wa Manchester United. Skysport.com

Klabu ya Sevilla FC imetinga fainali ya Ligi ya Ulaya (Europa League) baada ya kuiburuza Manchester United (2-1) huko Cologne, nchini Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Manchester United ndio walianza kuliona lango la   Sevilla kupitia mkwaju wa penalti kutoka kwa Bruno Fernandes katika dakika ya 9 ya mchezo.

Hata hivyo Sevilla ilikuja juu na kusawazisha kupitia mchezaji wake Suso  katika dakika ya 26 ya mchezo.

Mlinda mlango wa Sevilla Yassine Bounou aliiokoa timu yake na mikwaju kutoka kwa wachezaji wa Manchester Marcus Rashford, Bruno Fernandes, Mason Greenwood na Anthony Martial.

Katika dakika ya 78, Mholanzi Luuk de Jong aliipatishia klabu yake bao la ushindi. Klabu ya sevilaa ambayo imepata mataji mengi katika historia ya mashindano hayo na kushinda ubingwa wa michuano hiyo mara tano, itapepetana Agosti 21 katika fainali  na timu itakayoshinda katika nusu fainali itakayopigwa Agosti Agosti 17, kati ya Inter Milan na Shakhtar Donetsk.