MICHEZO-TENNIS

Daniil Medvedev kumenyana na Dominic Thiem

Kwa upande wa wanawake, Naomi Osaka kutoka Japan atamenyana na Victoria Azarenka kutoka Belarus katika hatua ya fainali.
Kwa upande wa wanawake, Naomi Osaka kutoka Japan atamenyana na Victoria Azarenka kutoka Belarus katika hatua ya fainali. REUTERS/Christian Hartmann

Daniil Medvedev kutoka Urusi leo anajitupa uwanjani kumenyana na Dominic Thiem raia wa Austria katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya mchezo ya Tennis, kuwania taji la mwaka huu la US Open kwa upande wa wanaume.

Matangazo ya kibiashara

Nusu fainali ya pili, Pablo Carreno Busta wa Uhispania atapambana na Alexander Zverev kutoka Ujerumani.

Kwa upande wa wanawake, Naomi Osaka kutoka Japan atamenyana na Victoria Azarenka kutoka Belarus katika hatua ya fainali.

Osaka alimshinda Mmarekani, Jeniffer Brady kwa seti za 7-6, 3-6 na 6-3, huku Azarenka akimbandua bingwa wa zamani Serena Williams kwa seti za 1-6, 6-3 na 6-3.