MOROCCO-CAF-MICHEZO

Uchaguzi wa rais wa CAF kufanyika Morocco

Uchaguzi wa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika utafanyika katika mji wa Rabat, Morocco.
Uchaguzi wa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika utafanyika katika mji wa Rabat, Morocco. Pline/Wilkimedia Commons

Mji wa Rabat nchini Morocco, utakuwa mwenyeji wa uchaguzi unaosubiriwa kwa hamu wa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika, utakaofanyika mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao cha Kamati tendaji ya Shirikisho hilo, iliyokutana kwa njia ya video siku ya Alhamisi.

Rais wa sasa Ahmad Ahmad amekataa kuweka wazi iwapi atawania tena nafasi hiyo au la, akisema uamuzi wa kuwania hauwezi kuwa wake peke yake, na kusisitiza kuwa kwa sasa kilicho mbele yake ni kumalizika kazi kabla ya uchaguzi huo.

Mbali na hilo, pamoja na mambo yaliyokubaliwa katika kikao hicho, na kutokana na shughuli za soka kutatiza kutokana na janga la Corona:-

-Michuano ya CHAN, inayowashirikisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani, itachezwa mwezi Januari mwaka 2021 kati ya tarehe 16 Januari hadi tarehe 7 Februari nchini Cameroon.

-Michuano ya CHAN mwaka 2022 itachezwa mwezi Januari mwaka 2023 na Algeria watakuwa wenyeji.

-Michuano ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho, itachezwa katikati ya mwezi Oktoba.

-Senegal itakuwa mwenyeji wa fainali ya soka la ufukweni