RIADHA-KENYA

Mwanariadha wa Kenya, Peres Jepchirchir, avunja rekodi ya dunia katika mbio za nusu marathon, Uholanzi

Mmoja ya wanariadha mashuhuri wa Kenya katika mbio za wanawake, Vivian Jepkemoi
Mmoja ya wanariadha mashuhuri wa Kenya katika mbio za wanawake, Vivian Jepkemoi Reuters/Damir Sagolj

Mkenya Peres Jepchirchir, amevunja rekodi yake siku ya Jumamosi wakati wa mashindano ya mbio za dunia za wanawake za nusu marathon zilizofanyika jijini Gdynia, Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Jepchirchir, mwenye umri wa miaka 27, alikimbia kwa muda wa saa 1, dakika 5 na sekunde 16.

Mjerumani, Melat Yisak Kejeta, alimaliza katika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 1, dakika 5 na sekunde 15, huku raia wa Ethiopia, Yalemzerf Yehualaw, akimaliza watatu kwa kutumia muda wa saa 1, dakika 5 na sekunde 19.

Katika mbio za wanaume, Mganda, Jacob Kiplimo alishinda mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika 58 na sekunde 49.

Katika mbio za wanawake, wote waliomaliza katika nafasi tatu za juu walishindana na Jepchirchir, wakati alipoweka rekodi ya saa 1, dakika 5 na sekunde 34 katika mashindano yaliyopita.

Kundi la kwanza la wakimbiaji, lilikimbia kilometa 10 kwa dakika 30 na sekunde 47, huku nafasi ya Muethiopia Ababel Yeshaneh na Mkenya, Joyciline Jepkosgei, ikipotea baada ya kupunguza mwendo katika mzunguko watatu na kujikuta wakimaliza kweye nafasi ya tano na sita kila mmoja.