JAPAN-IOC-MICHEZO

Michezo ya Olimpiki: IOC kuwapokea watazamaji Tokyo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki(IOC), Thomas Bach.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki(IOC), Thomas Bach. REUTERS

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (International Olympic Committee - IOC), Thomas Bach, amesema leo Jumatatu kuwa "ana imani" juu ya uwezekano wa kuwapokea watazamaji wa michezo ya Olimpiki ya Tokyo, iliyoahirishwa mwaka huu hadi msimu ujao wa joto kwa sababu ya mgogoro wa afya.

Matangazo ya kibiashara

Thomas Bach alikuwa akiongea baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japani Yoshihide Suga wakati anafanya ziara ya siku mbili huko Tokyo. Katika ziara hiyo Thomas Bach anatarajia kujadili na waandaaji wa mashindano hayo hatua za usafi zitakazochukuliwa kuzuia maambukizi ya Corona.

Hii ni ziara ya kwanza ya Thomas Bach nchini Japani tangu ile ya Machi iliyopita wakati mwenyekiti wa IOC na Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe walikubaliana kuahirisha Michezo ya Olimpiki kwa mwaka mmoja kwa sababu ya hatari za kiafya.

Yoshihide Suga, ambaye alichukua nafasi ya Shinzo Abe mnamo mwezi Septemba, amebaini kwamba nchi yake iko tayari kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka ujao, na kuongeza kuwa yuko tayari kufanya kazi na Thomas Bach na IOC juu ya maandalizi.