UINGEREZA-SOKA-MICHEZO

Pep Guardiola kuendelea kuinoa Manchester City, baada ya kusaini mkataba mpya

Pep Guardiola (Manchester City) katika mechi dhidi ya Tottenham, Aprili 17, 2019.
Pep Guardiola (Manchester City) katika mechi dhidi ya Tottenham, Aprili 17, 2019. © REUTERS/Phil Noble

Huko nchini Uingereza kocha wa klabu ya soka ya Manchester City Pep Guardiola, ametia saini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuifunza klabu hiyo hadi mwaka 2023.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyu wa Uhispania, anaendelea kutajwa kuwa kocha bora katika miaka ya hivi karibuni baada ya kushinda ligi kuu ya soka nchini Hispqniq, Ujerumani na nchini Uingereza akiwa na Manchester City mwaka 2017 na 2018.
Amekuwa kocha wa Manchester City tangu mwaka 2016.
Wakati huo huo kocha wa klabu ya Aston Villa Dean Smith amesema anataka ushahidi zaidi, kuonesha kuwa wanachezaji wapo katika hatari kubwa ya kupata majereha mabaya, kabla ya kuunga ;mkono kurejeshwa tena kwa wachezaji watano wa akiba, katika ligi kuu ya soka nchii humo.
Hata hivyo, makocha wengine kama Ole Gunna Shosa wa Manchetsrr United, Jurgun Kloop wa Liverrpool n Pep Guaridola wa Manchster City wanataka kurejeshwa kwa wachezaji hao kutokana na klabi hiwzo kuwa na mechi nyingi za kufuatana.