SOKA-AFRIKA-MICHEZO

Timu mbalimbali za soka Afrika kujitupa uwanjani Jumamosi na Jumapili

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza kuwa fainali ya mwaka huu ambayo ni ya 29 kuwania taji la CAF Super Cup, itachezwa jijini Cairo nchini Misri na sio Qatar, kutokana na mabadiliko ya wakati wa kufanyika kwa fainali hiyo ambayo ilikuwa imefanyike mwezi Agosti.

baada ya wiki mbili za michuano ya soka baina ya taimu za taifa kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon, michuano ya ligi kuu inarejea katika mataifa machache ya Afrika ambayo yameruhusu kuendelea kwa mashindano hayo.
baada ya wiki mbili za michuano ya soka baina ya taimu za taifa kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon, michuano ya ligi kuu inarejea katika mataifa machache ya Afrika ambayo yameruhusu kuendelea kwa mashindano hayo. REUTERS/Nigel Roddis
Matangazo ya kibiashara

Fainali ya mwaka huu itawakutanisha mabingwa wa taji la klabu bingwa barani Afrika, ambaye anasubiriwa kati ya Ahly na Zamalek, zote za Misri zitakazokutana tarehe 27 mwezi huu na mshindi atamenyana na RS Berkane ya Morocco katika fainali hiyo ya Super Cup.

Hayo yakijiri baada ya wiki mbili za michuano ya soka baina ya taimu za taifa kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon, michuano ya ligi kuu inarejea katika mataifa machache ya Afrika ambayo yameruhusu kuendelea kwa mashindano hayo.

Nchini DRC, mechi kadhaa za ligi kuu zimepangwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili.

Siku ya Jumamosi, huko Kindu, klabu ya Maniema Union itakuwa mwenyeji wa Groupe Bazano.
Siku ya Jumapili, Simba FC itachuana na Blessing FC katika uwanja wa Kibasa Maliba, TP Mazembe itachuana na Saint Eloi Lupopo, huku AS Vita Club ikimenyana na DC Motema Pembe jijini Kinshasa.

Nchini Tanzania, uongozi wa klabua ya Yanga SC umemteua Mkurugenzi wake wa Fedha, Haji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo , akichukua nafasi ya Wakili Simon Patrick aliyesimamishwa kazi.

Michuano ya ligi kuu Tanzania bara nayo imepangwa mwishoni mwa wiki hii, kesho Jumamosi Coastal Union watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi Simba Sports Club, huku KMC watacheza na Azam FC.