FUFA-CAF-AHMAD-SOKA-MAADILI-UCHUMI

CAF: Rais Ahmad asimamishwa kazi kwa miaka mitano na FIFA

Tume ya Maadili ya Fifa imemsimamisha kazi rais wa Shirikisho la Soka Afrika Ahmad kwa miaka mitano.
Tume ya Maadili ya Fifa imemsimamisha kazi rais wa Shirikisho la Soka Afrika Ahmad kwa miaka mitano. CRISTINA ALDEHUELA / AFP

Tume ya Maadili ya shirikisho la Soka Duniani, FIFA imemsimamisha kazi rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na makamu wa rais wa FIFA kwa miaka mitano, huku akitozwa faini ya euro 185,000, hasa kwa ubadhirifu.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka 30 Issa Hayatou akiliongoza Shirikisho la Soka Afrika, Bw. Ahmad, raia wa Madagascar, aliyechaguliwa kwa mshangao wa kila mtu mwezi Machi 2017, alitarajiwa kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa soka katika bara la Afrika.

Karibu miaka minne baadaye, rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Afrika Ahmad amesimamishwa kazi kwa miaka mitano na Tume ya Maadili ya shirikisho la Soka Duniani, FIFA, ambayo imemtaka alipe faini ya euro 185,000.

Ahmad pia aliwekwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za ufisadi mnamo mwezi Juni 2019 jijini Paris, nchini Ufaransa.

Kulingana na taarifa ya FIFA: "Bw. Ahmad amearifia kuhusu uamuzi huo leo (Novemba 23, 2020), wakati marufuku hiyo ilipoanza kutumika. "

"Bwana Ahmad alishindwa kutekeleza jukumu lake la uaminifu"

Bw. Ahmad, aliyezaliwa Desemba 30, 1959 nchini Madagascar, na mwanasiasa wa zamani, ambaye alihudumu kama Katibu dola anayeshusika na masuala ya Michezo na Waziri wa Uvuvi nchini Madagascar, "ana hatia ya kukiuka Vifungu vya 15 (Wajibu wa uaminifu), 20 (Kukubali na kusambaza zawadi au faida zingine) na 25 (Matumizi mabaya ya utawala) vya toleo la mwaka 2020 la Kanuni za Maadili za FIFA, pamoja na Ibara ya 28 (Matumizi mabaya ya fedha) ya toleo la mwaka 2018 ".

"Uchunguzi wa tabia ya Bwana Ahmad kama rais wa CAF kati ya mwaka 2017 na 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Makkah ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , imesema taarifa ya FIFA.

Hata hivyo Bw. Ahmad amefutlia mbali tuhuma dhidi yake, akibaini kwamba ni uzushi mtupu.