SOKA-UEFA-ULAYA

Ligi ya Mabingwa: PSG na Basaksehir waondoka uwanjani baada ya matamshi ya kibaguzi

Mechi ya klabu bingwa barani Ulaya  Paris St Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir F.K.
Mechi ya klabu bingwa barani Ulaya Paris St Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir F.K. Reuters

Timu za Paris SG na Basaksehir Istanbul kutoka Uturuki zinatarajia kumenyana leo Jumatano Desemba 9, baada ya mechi yao kuahirishwa Jumanne wiki hii kutokana na matamshi ya kibaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya Paris SG na Basaksehir Istanbul kutoka Uturuki ilisitishwa katika dakika ya 16 Jumanne, Desemba 8 na wachezaji walirudi kwenye chumba cha kubadilishia nguo, baada ya tukio linalodaiwa kuwa la kibaguzi lililomhusisha mwamuzi wa nne wa mchezo huo.

Tukio hilo ni la kwanza kushuhudiwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa. Mechi hiyo iliahirishwa hadi leo Jumatano, Desemba 9 saa 1:55 usiku, saa za Afrika ya Kati (sawa na saa 2:55 usiku, saa za Afrika Madshariki).

Mechi hii itapigwa kwenye uwanja wa soka wa Parc des Princes. Siku ya sita na ya mwisho ya hatua ya makundi, katika dakika ya 23, wachezaji wa klabu ya Basaksehir Istanbul waliondoka uwanjani na kuelekea katika chumba cha kubadilishia nguo, baada ya dakika kadhaa za majadiliano pembezoni mwa uwanja.

Mechi ilisitishwa katika dakika ya 16 baada ya tukio linalodaiwa kuwa la kibaguzi lililomhusisha mwamuzi wa nne wa mechi hiyo.

Pierre Achille Webo, Kocha msaidizi wa klabu ya Basaksehir Istanbul, alishutumu matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na mwamuzi wa nne dhidi yake.

Hali hiyo imesababisha viongozi wa Uturuki, ikiwa ni pamoja na rais wa Uturuki kulaani matamshi hayo yaliyodaiwa kutolewa na mwamuzi wa nne.  

Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA, linatarajia kufungua uchunguzi haraka. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan pia ameshtumu matamshi yenye ubaguzi wa rangi na kutoa wito kwa UEFA kuchukua hatua. "Sina mashaka kwamba UEFA itachukua hatua zinazohitajika," Erdogan ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wakati huo huo, klabu ya Leipzig, imefuzu katika hatua ya 8 kwa kuifunga Manchester United 3-2.