RWANDA

Uganda na Tanzania kujitupa uwanjani kuwania taji la CECAFA

Timu ya taifa ya soka ya Uganda.
Timu ya taifa ya soka ya Uganda. @OfficialFUFA

Uganda na Tanzania zitachuana baadaye leo kuwania taji la CECAFA kwa vijana wasiozidi miaka 17, katika fainali itakayochezwa katika uwanja wa Umuganda huko Rubavu nchini Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Tanzania ilifuzu katika hatua ya fainali baada ya kuishinda Ethiopia manbao 4-3 kupitia mikwaju ya Pënalti, lakini Uganda nao walishinda Djibouti bao 1-0.

Kabla ya mechi hiyo ya fainali, Djibouti na Ethiopia zitachuana kumtafuta mshindi wa tatu.

Tayari Uganda na Tanzania zimefuzu kuiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya bara Afrika italkayofanyika mwaka 2021 mwezi Julai.