CAF-TP MAZEMBE-AL HILAL

Al Hilal na TP Mazembe yashindwa kufungana mechi ya klabu bingwa

Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe  Joel Kimwaki.
Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe Joel Kimwaki. CARL DE SOUZA / AFP

Klabu ya Al Hilal ya Sudan na TP¨Mazembe ya Jamhuri ya Kidempkrasia ya Congo, zilishindwa kufungana katika mechi muhimu, hatua ya makundi, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo ya kundi B, ilichezwa katika mji wa Omdurman, siku ya  Jumatano usiku.

Matokeo haya, yanaifanya TP Mazembe sasa kuwa na alama mbili katika kundi hili, baada ya kupata matokeo kama hayo na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria katika mechi yake ya ufunguzi.

Al Hilal walishindwa kutumia nafasi  nyingi walizopata kupata mabao, licha ya kutumia pasi fupifupi, kuwachanganya wapinzani wake, huku kipindi cha pili, TP Mazembe wakitawala mchezo.

Hata hivyo, Al Hilal nayo ilipata alama yake ya pili baada ya mechi yake ya kwanza kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.