CAF-SOKA-VIJANA

Droo ya michuano ya soka baina ya vijana wasiozidi miaka 17 yawekwa wazi

Droo ya michuano ya soka barani Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 itakayofanyika nchini Morocco
Droo ya michuano ya soka barani Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 itakayofanyika nchini Morocco © https://www.cafonline.com/

Droo ya michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, itakayofanyika kati ya tarehe 13 hadi 31 nchini Morocco imetangazwa.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, yatawakilishwa na Uganda na Tanzania katika mashindano hayo.

Kuna makundi matatu kuelekea fainali hii ya bara Afrika, kutafuta taji hili.

Kundi A: Morocco, Uganda, Zambia, Cote d'Ivoire

Kundi B: Nigeria, Tanzania, Algeria, Congo

Kundi C: Cameroon, Senegal, Mali, Afrika Kusini

Michuano hiyo itachezwa katika miji ya Rabat na Casablanca.

Mabingwa watetezi ni Cameroon.