SOKA- KLABU BINGWA AFRIKA 2021

Simba SC miongoni mwa klabu tano zilizofuzu hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika

Taji la klabu bingwa barani Afrika
Taji la klabu bingwa barani Afrika MOHAMED EL-SHAHED / AFP

Klabu tano za mchezo wa soka, tayari zimefuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika mechi moja kabla ya kumalizika kwa michuano ya hatua ya makundi msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa klabu hizo ni pamoja na Simba Sports Club ya Tanzania, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Al Ahly ya Misri.

Nyingine ni Wydad Casablanca ya Morocco na Esperance de Tunis ya Tunisia.

Simba SC ilijihakikishia nafasi hiyo kutoka kundi A, baada ya kuishinda AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuifunga mabao 4-1 na kuongoza kundi hilo kwa alama 13 baada ya mechi tano.

Al Ahly nayo ni ya pili katika kundi hilo la A kwa alama nane, na tayari imefuzu licha ya sare ya mabao 2-2 na Al Merrikj ya Sudan.

Kundi B, mbali na Mamelodi Sundowns ambayo ina alama 13, CR Belouizdad ya Algeria au Al Hilal ya Sudan zina nafasi ya kufuzu. CR Belouizdad ina alama sita, huku Al Hilali ikiwa na alama nne. Mechi ya mwisho, Aprili 9, Al Hilal itamenyana na TP Mazembe huku CR Belouizdad  itamenyana na Mamelodi Sundowns.

Kibarua kigumu kipo katika ku,di C, kati ya Horoya ya Guinea na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.Klbau zote zina alama nane, na yeyote anaweza kufuzu, kuungana na Wydad Casablanca.

Mechi ya tarehe 10 Aprili kati ya Horoya na Kaizer Chiefs itakuwa kama fainali ya kundi hilo katika kundi hilo na mechi hiyo itachezwa jijini Conakry. Mechi ya Kwanza, timu zote hazikufungana.

 

Kundi D, MC Alger ya Algeria na Zamalek ya Misri, zinapambana kufuzu. MC Alger ambayo ina alama nane, itachuana na Esperance de Tunis, katika mechi ya mwisho tarehe 10 mwezi Aprili.

Huku Zamalek ambayo ina alama tano, ikijiandaa kukabiliana na Teungueth ya Senegal kwa ambayo tayari imeshandolewa katika michuano hiyo.