LIGI YA MABINGWA

Ligi ya Mabingwa: Manchester City yatinga fainali kwa kuifungia PSG

Winga wa Manchester City Riyad Mahrez anafunga bao la kwanza kati ya mawili dhidi ya PSG kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali  wa Ligi ya Mabingwa.
Winga wa Manchester City Riyad Mahrez anafunga bao la kwanza kati ya mawili dhidi ya PSG kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali wa Ligi ya Mabingwa. AFP - PAUL ELLIS

Manchester City imetinga fainali ya kwanza kabisa ya Ligi ya Mabingwa Mei 4, 2021, baada ya kuifunga Paris Saint-Germain 2-0 katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali (2-1 katika mchezo wa kwanza).

Matangazo ya kibiashara

Klabu hiyo ya Uingereza itamenyana na mshindi wa kati ya Chelsea- na Real Madrid Mei 29 huko Istanbul.

Paris Saint-Germain (PSG) haitacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa pili mfululizo. Klabu hiyo ya Ufaransa iliondolewa na Manchester City katika nusu fainali ya Kombe la Ulaya Mei 4, 2021 Kaskazini mwa Uingereza.

PSG imepoteza 2-0 kwenye uwanja wa Manchester City, uliyokumbwa na mvua ya mawe. Katika mechi ya kwanza PSG walipoteza baada ya kubamizwa 2-1.