SOKA-LIGI YA MABINGWA

Ligi ya Mabingwa: Chelsea kumenyana na Manchester City katika fainali

Bao la Chelsea likifungwa na Timo Werner dhidi ya Real Madrid, katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Bao la Chelsea likifungwa na Timo Werner dhidi ya Real Madrid, katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. AFP - GLYN KIRK

Chelsea itamenyana na Manchester City katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Mei 29, 2021 huko Istanbul, nchini Uturuki. Klabu hiyo ya Uingereza iliifunga Real Madrid mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali Jumatano hii Mei 5 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Real Madrid watalazimika kusubiri ili kushinda Kombe lao la kumi na nne la Ligi ya Mabingwa. Klabu hiyo ya Uhispania iliondolewa katika nusu fainali ya Kombe la kifahari la soka la Ulaya Mei 5, 2021 huko London.

Real Madrid walifungwa mabao 2-0 na Chelsea ambao walikuwa tayari wamewashikilia nafasi nzuri katika mechi ya kwanza (1-1).

Katika kipindi cha kwanza, hata hivyo, kila timu ilipata fursa zake nzuri na za wazi lakini bao la kwanza la klabu hiyo ya Uingereza lilifungwa katika dakika ya 28 ya mchezo.

Bao la pili lilifungwa katika dakika ya 85 ya kipindi cha pili cha mchezo, na mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Chelsea kwa mabao 2-0.