DRC-SOKA

Timu ya taifa ya soka ya DRC yampata kocha mpya Hector Cuper

Timu ya taifa ya DRC, Léopards, imempata kocha mpya, Hector Cuper, raia wa Argentina.
Timu ya taifa ya DRC, Léopards, imempata kocha mpya, Hector Cuper, raia wa Argentina. Photo MONUSCO/John Bompengo

Kocha wa siku nyingi wa Argentina Hector Cuper ametajwa kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Matangazo ya kibiashara

Cuper mwenye umri wa miaka 65 ana kazi kubwa ya kuisaidia Leopard kufuzu kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar. 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepangwa katika kundi moja na Benin, Madagascar na Tanzania na mechi hizo zitaanza kuchezwa mwezi Septemba. 

Aliwahi kuifunza Misri na kuisaidia kufuzu kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi. 

Cuper amewahi pia kufunza soka katika klabu mbalimbali nchini Italia na Uhspania. 

Kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa DRC alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Uzbekistan.