KENYA-JUDO

Shirikisho la mchezo wa Judo barani Afrika wapata viongozi wapya

Shirikisho la mchezo wa Judo barani Afrika limewapata viongozi wapya, ambao ni Mkenya Shadrach Maluki (mwenyekiti) na Thierry Siteny kutoka  Madagascar ambaye amechaguliwa kuwa rais wa Muungano wa mchezo huo barani Afrika.
Shirikisho la mchezo wa Judo barani Afrika limewapata viongozi wapya, ambao ni Mkenya Shadrach Maluki (mwenyekiti) na Thierry Siteny kutoka Madagascar ambaye amechaguliwa kuwa rais wa Muungano wa mchezo huo barani Afrika. © Judo Africa

Shadrach Maluki kutoka nchini Kenya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa shirikisho la mchezo wa Judo barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kufanyika kwa uchaguzi jijini Dakar nchini Senegal.

Baada ya kuchaguliwa kwa Maluki, amesema kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa mchezo wa Judo unafahamika barani Afrika.

Thierry Siteny kutoka  Madagascar naye amechaguliwa kuwa rais wa Muungano wa mchezo huo barani Afrika.

Wawili hao watakuwa katika nyadhifa hizo kwa miaka mitano ijayo.