BRAZILI-SOKA

Michuano ya Copa America kuanza Juni 13

Mpaka sasa haijafahamika ni viwanja vipi vitatumika kuandaa michuano hiyo iwapo mashindano hayo yataendelea kwa sababu Brazil pia inakabiliwa na janga kubwa la Corona.
Mpaka sasa haijafahamika ni viwanja vipi vitatumika kuandaa michuano hiyo iwapo mashindano hayo yataendelea kwa sababu Brazil pia inakabiliwa na janga kubwa la Corona. DANIEL MUNOZ AFP/File

Brazil imetajwa kuwa mwenyeji mpya wa mashindano ya mchezo wa soka, kuwania taji la Copa America, wiki mbili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo iliyopangwa kuanza Juni 13.

Matangazo ya kibiashara

Awali Argetina ndio iliyokuwa imepewa nafasi ya kuwa mwaandaji lakini kutokana na janga la virusi vya Corona nchini humo, ikapokonywa nafasi hiyo.

Mpaka sasa haijafahamika ni viwanja vipi vitatumika kuandaa michuano hiyo iwapo mashindano hayo yataendelea kwa sababu Brazil pia inakabiliwa na janga kubwa la Corona