MICHEZO-TENNIS

Naomi Osaka ajiondoa kwenye mashindano ya French Open

Naomi Osaka, bingwa mara nne wa mataji makubwa ya mchezo wa Tennis.
Naomi Osaka, bingwa mara nne wa mataji makubwa ya mchezo wa Tennis. MARTIN BUREAU AFP

Bingwa nambari mbili duniani katika mchezo wa Tennis kwa upande wanawake, Naomi Osaka kutoka Japan amejiondoa kwenye mashindano ya mwaka huu ya French Open.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya bingwa huyo kukataa kuzungumza na vyombo vya Habari wakati wa mashindano hayo, kwa kile anachosema amekuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo anapoulizwa maswali na wanahabari.

Bingwa huyo mara nne wa mataji makubwa ya mchezo huo, kabla ya kujindoa kwenye michuano hii, siku ya Jumapili, alitozwa faini ya Dola 15,000 kwa kukataa kuhojiwa na wanahabari baada ya mchuano wake wa kwanza dhidi ya Patricia Maria Tig kutoka Romania.