SOKA-EURO 2020

Michuano ya Euro hatimaye kuanza kutifua vumbi barani Ulaya

Taji la Euro 2020
Taji la Euro 2020 Fabio FRUSTACI ANSA/AFP/File

Michuano ya soka kuwania taji la bara Ulaya maarufu kama Euro 2020, iliyoahirishwa kutoka mwaka 2020 hadi mwaka 2021 inaanza siku ya Ijumaa nchini Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya kwanza ni kati ya mabingwa wa zamani Italia na Uturuki, jijini Instanbul.

Kutokana na janga la Covid 19, mashabiki wanaotarajiwa kushuhudia michuano hii ni robô ya idadi ya kawaida.

Mabingwa watetezi Ureno, wamepangwa katika kundi moja na Hungary na mabingwa wa zamani Ufaransa na Ujerumani.

Mara ya mwisho kwa mashindano haya yanayofanyika kila baada ya miaka nne kufanyika ilikuwa ni mwaka 2016.

 

Muhimu

Mashindano haya yanaanza Ijumaa, Juni 11.

Michuano ya mwondoano itaanza Juni 26.

Fainali itachezwa Julai 11 katika uwanja wa Wembley, jijini London.

 

Mashindano haya yanafanyika wapi ?

Kwa mara ya kwanza, mashindano haya yanafanyika katika miji 11 ambayo ni London, Saint Petersburg, Baku, Munich, Rome, Amsterdam, Bucharest, Budapest, Copenhagen, Glasgow na Seville.

 

Timu ngapi zinashiriki

Kuna timu 24 zinazoshiriki, zimegawanywa katika makudni sita. Kutakuwa na mechi 51.

Kundi A: Uturuki, Italia, Wales, Switzerland

Kundi B: Denmark, Finland, Ubelgiji, Urusi

Kundi C: Uholanzi, Ukraine, Austria, Macedonia Kaskazini

Kundi D: Uingereza, Croatia, Scotland, Jamhuri ya Czech

Kundi E: Hispania, Sweden, Poland, Slovakia

Kundi  F: Hungary, Ureno , Ufaransa, Ujerumani.

 

Mfumo wa mashindano

Timu mbili kutoka kila kundi, pamoja na timu nne bora zitakazokuwa zimemaliza katika nafasi bora za tatu, zitafuzu katika hatua ya robo fainali itakayokuwa na timu 16.

 

Mashabiki wataruhusiwa uwanjani ?

Ndio. Viwanja vyote 11 vimeruhusiwa kuwa na mashabiki.Shirikisho la soka barani Ulaya limeeleza kuwa viwanja kama Saint Petersburg na Baku, vitakuwa na asilimia 50 ya mashabiki.

Lakini viwanja vya Amsterdam, Bucharest, Copenhagen, Glasgow, Rome na Seville vikitarajiwa kuwa na kati ya  asilimia  25 hadi 45 ya mashabiki.

London asilimia 25, Munich 22 na Budapest inatarajiwa kuwa na kairbu asilimia 100.