UFARANSA - UJERUMANI EURO 2020

Ufaransa yashinda mechi ya sita mfululizo katika uwanja wa Munich nchini Ujerumani

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba (kushoto) akizungumza na beki wa Ujerumani Antonio Ruediger wakati wa mechi yao ya Euro 2020 huko Munich
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba (kushoto) akizungumza na beki wa Ujerumani Antonio Ruediger wakati wa mechi yao ya Euro 2020 huko Munich Matthias Schrader POOL/AFP

Timu ya taifa ya Ufaransa les Blues wameshinda mechi yao ya kwanza katika michuano ya Euro-2021 jana Jumanne. Timu ya Ufaransa iliweza kupinga changamoto ya mashambulizi kutoka timu ya taifa ya Ujerumani kushinda bao dhidi ya kambi yao ya Hummels (1-0).

Matangazo ya kibiashara

Les Blues waliteseka lakini walishinda, Jumanne, Juni 15, mechi yao ya kwanza ya Euro-2020. Katika mpambano huu wa kwanza katika kundi la kifo, timu ya Ufaransa iliibuka mshindi dhidi ya Ujerumani kwenye Uwanja wa Allianz Arena huko Munich. Bao dhidi ya kambi yake ya Hummels kwenye mkwaju kutoka kwa Hernandez ulitoa ushindi kwa vijana wanaonolewa na kocha Didier Deschamps.

Mshambuliaji Karim Benzema na Klian Mbappe walifunga mabao ambayo yalikataliwa.

Katika hatuwa ,nyingine Ureno imeanza vyema Euro 2020 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Hungary katika mchezo wa Kundi F katika Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest.

Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Raphaël Guerreiro dakika ya 84 na Nahodha Cristiano Ronaldo dakika ya 87 kupitia mkwaju wa ka penalti na 90 na ushei akimalizia pasi ya Rafa Silva.

Ronaldo anakuwa mfungaji wa mabao mengi kihistoria kwenye fainali za Kombe hilo la Mataifa ya Ulaya, 11 akimpiku Mfaransa Michel Platini