SOKA-DRC

Rais wa soka nchini DRC ajiuzulu

Rais wa Shirikisho la soka nchini DRC Constant Omari Selemani
Rais wa Shirikisho la soka nchini DRC Constant Omari Selemani © fecofa

Constant Omari Selemani, amejiuzulu kama rais wa Shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FECOFA).

Matangazo ya kibiashara

Omari mwenye umri wa miaka 63, ameachia nafasi hiyo baada ya kuhudumu kama kiongozi wa soka nchini humo kwa miaka 18.

Tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2003, mbali na kuhudumu kama rais wa FECOFA, kwa nyakati tofauti, aliwahi pia kuhudumu katika Kamati kuu ya Shirikisho la soka barani AFrika CAF na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Amesema angejiuzulu mapema, baada ya timu ya taifa kuondolewa kwenye michuano ya kufuzu kucheza fainali ya mataifa ya Afrika mwaka 2021, lakini akaamua kuendelea na majukumu ya kumtafta kocha mpya.

Nimekuwa rais wa FECOFA tangu mwaka 2003, nimehudumu kwenye Kamati ya CAF na FIFA nafikiri wakati umefika wa kukabidhi madaraka,”  alisema mwezi Machi.

Omari ambaye pia aliwahi kuhudumu kama rais wa muda wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF kati ya mwezi Novemba 2020 mpaka mwisho wa Januari mwaka 2021, ameondoka wakati huu uchaguzi wa kumpata rais mpya unapotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.