JAPAN-MICHEZO

Michezo ya Olimpiki kufunguliwa katikati mwa janga la Corona Tokyo

Mji unaoandaa michezo hiyo wa Tokyo unawekwa katika hali ya tahadhari kutokana na idadi kubwa ya maambukizi huku karibu thuluthi mbili ya raia wa Tokyo wakisema kamati andalizi ya Olimpiki haiwezi kudhibiti maambukizi michezo hiyo inapoendelea.
Mji unaoandaa michezo hiyo wa Tokyo unawekwa katika hali ya tahadhari kutokana na idadi kubwa ya maambukizi huku karibu thuluthi mbili ya raia wa Tokyo wakisema kamati andalizi ya Olimpiki haiwezi kudhibiti maambukizi michezo hiyo inapoendelea. Philip FONG AFP

Baada ya kuahirishwa kwa mwaka mmoja, Michezo ya Olimpiki ya 32 ya enzi ya kisasa inafunguliwa Tokyo, Ijumaa hii, katika hali ya sintofahamu. Janga la Covid-19 bado lina uzito mkubwa juu ya hafla hii, na kati ya mgogoro wa kiafya na matokeo yake mabaya, Japan yasherehekea shingo upande.

Matangazo ya kibiashara

Uwanja mpya wa Olimpiki wa Tokyo, uliokamilishwa mwishoni mwa mwaka wa 2019, uligharimu wastani wa Bilioni 1.2 hadi euro Bilioni 1.8.  Uwanja huu wa kisasa vuna uwezo wa kupokea watu 68,000.

Tayari michezo hii ya olimpiki iliahirishwa kwa mwaka mmoja. Na mamlaka ya Japan, katika kukabiliana na aina mpya ya kirusi cha Corona (Delta), hali ya hatari ilitangazwa Julai 12.

Tokyo yawekwa katika hali ya tahadhari

Mji unaoandaa michezo hiyo wa Tokyo unawekwa katika hali ya tahadhari kutokana na idadi kubwa ya maambukizi huku karibu thuluthi mbili ya raia wa Tokyo wakisema kamati andalizi ya Olimpiki haiwezi kudhibiti maambukizi michezo hiyo inapoendelea.

Katika taarifa inayofungamana na suala hilo ni kwamba timu ya kandanda ya Afrika Kusini haifahamu iwapo itacheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Japan baada ya sheria za kuzuia maambukizi ya Covid 19 kupelekea wachezaji pamoja na makocha 21 kuwekwa karantini. Waandalizi wa michezo hiyo ya olimpiki wamethibitisha kwamba waliokutana karibu na timu hiyo ya Afrika Kusini wamewekwa karantini.