JAPAN-MICHEZO

Michezo ya Olimpiki: Medali 21 za dhahabu kushindaniwa katika michezo mbalimbali

Ahmed Hafnaoui, Mtunisia, bingwa mpya wa Olimpiki katika mchezo wa kuogelea wa mita 400 katika Michezo ya Tokyo.
Ahmed Hafnaoui, Mtunisia, bingwa mpya wa Olimpiki katika mchezo wa kuogelea wa mita 400 katika Michezo ya Tokyo. REUTERS - KAI PFAFFENBACH

Leo Jumatatu ni siku ya tatu ya Michezo ya Olimpiki, inayoendelea jijini Tokyo nchini Japan. Kuna medali 21 za dhahabu za kushindaniwa kwenye michezo mbalimbali hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Tayari, Adam Peaty, imeinyakulia Uingereza medali ya kwanza ya  dhahabu katika mchezo wa kuogelea Mita 100 mtindo wa breastroke na kutetea medali hiyo aliyoshinda mwaka 2016.

Baadhi ya matokeo ya leo:

Brazil imeishinda Kenya kwa seti 2 kwa 0 za 21, 15, 21, 9  kwenye mchezo wa wavu kwa upande wa wanawake unaochezwa ufukweni.

 Katika mchezo wa raga kwa upande wa wanaume, wachezaji saba kila upande, mechi ya ufunguzi Kenya wamefungwa na Marekani 19 kwa 14 katika kundi C na baadaye itacheza na Afrika Kusini.

Afrika Kusini nayo imeishinda Ireland, kwa alama 33 kwa 14.

Masumbwi

Ssemuju Kavuma David wa Uganda, atamenyana na Nemouchi Younes wa Algeria, katika hatua ya 32 uzani wa kati ya 69-75.

Tshama Mwenekabwe David wa DRC atapambana na Seyi Dieudone Wilfred wa Cameroon.