Burundi kumenyana na Tanzania Ijumaa Julai 30

Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba.
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba. RFI-KISWAHILI

Tanzania na Burundi, zitamenya katika fainali ya kuwania taji la mchezo wa soka kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Bahir Dar huko Ethiopia.

Matokeo ya mechi za nusu fainali siku ya Jumanne:

Tanzania 1 Sudan Kusini 0

Burundi 4 Kenya 2 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya kutofungana katika muda wa kawaida.

Kenya na Sudan Kusini, zitamenyana kutafuta mshindi wa tatu katika michuano hii.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Chalenji (CECAFA)
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Chalenji (CECAFA) Online