UGANDA-SOKA

Micho Sredojevic arejeshwa tena Uganda kuendelea kuinoa Cranes

Timu ya taifa ya soka ya Uganda.
Timu ya taifa ya soka ya Uganda. FADEL SENNA / AFP

Shirikisho la soka nchini Uganda (Fufa), limetangaza kumrejesha tena Mserbia Micho Sredojevic, kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka, Cranes.

Matangazo ya kibiashara

Micho amesaini mkataba wa miaka mitatu na ataanza rasmi kazi tarehe 1 mwezi Agosti.

Aliondoka nchini Uganda, baada ya fainali ya mataifa ya Afrika 2017 kufuatia mvutano wa kutolipwa mshahara wake.

Kazi kubwa inayomsubiri ni kuiandaa Uganda kuelekea mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2022.

Uganda imepangwa pamoja na majirani Kenya, Rwanda na Mali.

Kabla ya kurejea Uganda, Micho amekuwa akifunza soka nchini Zambia kabla ya kuamua kuondoka.