SOKA-MAN UNITED

Soka: Cristiano Ronaldo aondoka Juventus na kujiunga tena na Manchester United

Cristiano Ronaldo ametwaa kiatu cha dhahabu cha mashindano ya Euro 2020 baada ya kuibuka mfungaji bora wa mashindano.
Cristiano Ronaldo ametwaa kiatu cha dhahabu cha mashindano ya Euro 2020 baada ya kuibuka mfungaji bora wa mashindano. REUTERS - TOBY MELVILLE

Klabu ya Manchester United imefikia mkataba na Juventus kuhusu uhamisho wa nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo Ijumaa hii, Agosti 27. Kiasi cha fedha na muda wa mkataba bado haujafamishwa

Matangazo ya kibiashara

Manchester City ni moja ya vilabu ambavyo viliwasiliana na wakala wa Ronaldo Jorge Mendes, na ripoti zingine zinaonyesha kuwa masharti ya kibinafsi tayari yamekubaliwa

Cristiano Ronaldo amerudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United, miaka 12 baada ya kuondoka katika timu hiyo. Cristiano Ronaldo anarudi Manchester United ambapo alicheza kwa misimu sita kati ya 2003 na 2009.

"Cristiano ni nguzo wa klabu hii. Ni mchezaji mkubwa kwa maiak yote kama mnataka maoni yangi, ”amesema kocha wa Mashetani Wekundu Ole Gunnar Solksjaer, ambaye alicheza naye misimu minne.