KLABU BINGWA AFRIKA-SOKA-WANAWAKE

Fainali ya klabu bingwa Afrika kwa wanawake kuchezwa Misri

Fainali kati ya klabu ya Hasaacas Ladies kutoka Ghana dhidi ya  Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Novemba 19 2021
Fainali kati ya klabu ya Hasaacas Ladies kutoka Ghana dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Novemba 19 2021 © CAFwomen

Fainali ya kwanza kuwania taji la mchezo wa soka kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake, inachezwa baadaye siku ya Ijumaa katika uwanja wa June 30 jijini Cairo nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo utawakutanisha Hasaacas Ladies kutoka Ghana dhidi ya  Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Hasaacas Ladie ilifanikiwa kufika katika hatua ya fainali baada ya kuishinda AS FAR ya Morocco kwa mabao 2-1 huku Mamelodi Sundowns ikailaza Malabo Kings kwa mikwaju 5-4 ya penalty baada ya mechi hiyo kumalizika kwa kutofungana katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

 

Tayari kombe la kwanza litakalokabidhiwa kwa mshindi, limewasili jijini Cairo.

Mshindi wa tatu ni AS FAR, iliishinda Malabo Kings mabao 3-1.

Klabu nane zilishiriki kwenye fainali hii ya kwanza.

Kundi A : Hasaacas Ladies (Ghana), Malabo Kings(Equatorial Guinea), Wadi Delga (Misri), AS Mande (Mali)

Kundi B: Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), AS FAR (Morocco), Rivers Angels (Nigeria), Vihiga Queens (Kenya).