KRIKETI-AFRIKA KUSINI

Mchezaji maarufu wa Cricket nchini Afrika Kusini AB de Villiers astaafu

Mchezaji wa Afrika Kusini AB de Villiers aliyetangaza kustaafu mchezo wa Tennis
Mchezaji wa Afrika Kusini AB de Villiers aliyetangaza kustaafu mchezo wa Tennis Manjunath KIRAN AFP

Mchezaji wa Afrika Kusini katika mchezo wa Cricket, Abraham Benjamin de Villiers, ametangaza kustafu kucheza  na kujihusisha na shughuli zote za mchezo huo.

Matangazo ya kibiashara

De Villiers mwenye umri wa miaka 37, aliye na uzoefu mkubwa katika mchezo huu amesema amefikia uamuzi huo kwa sababu mwenge wake, kwenye mchezo huu, hau’ngai tena.

Tangu mwaka 2004, alikuwa anaichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini hadi mwaka 2018, na kwa kipindi hicho, amecheza mechi 114 aina ya Test yanayodumu kwa siku tano.

Mechi 228 za ODIs na mechi 78 za Kimataifa aina ya T20.