Soka: Mwaka mmoja kuelekea kombe la dunia nchini Qatar
Imechapishwa:
Ni mwaka mmoja kuelekea michuano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka nchini Qatar mwaka 2022.
Maandalizi yamefika katika hatua ya lala salama, ikiwa ni pamoja na viwanja kuwa tayari na miundo mbinu mingine muhimu kama makaazi ya wageni.
Mashabiki zaidi ya Milioni 1 kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, wanaotarajiwa kuhudhuria michuano hiyo ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza nchini Qatar.
Tarehe 21 mwezi Novemba mwaka 2022, jiji la Doha litakuwa mwenyeji wa mashindano haya makubwa duniani, pamoja na miji mingine kama Lusail, Al Khor, Al Rayyan na Al Wakrah.
Qatar iliingia kwenye historia ya mchezo wa soka duniani mwaka 2010 baada ya kuishinda Marekani kuwa mwenyeji wa kombe la duniai, katika mazingira ambayo yalidaiwa kuwa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati ilinunua kura ili kushinda nafasi hiyo.
Mataifa 32 yatashiriki katika michuano hiyo, bara la Afrika likiwakilishwa na mataifa matano.