TENNIS-CHINA

Tennis: Serena ataka mchezaji wa China Peng Shuia kutetewa.

Mcheaji wa Tennis kutoka China  Peng Shuai
Mcheaji wa Tennis kutoka China Peng Shuai GREG BAKER AFP/File

Mchezaji wa mchezo wa Tennis kutoka nchini Marekani, Serena Williams, amesema madai ya mchezaji wa China Peng Shuia, ya kunyanyaswa kimapenzi na afisa wa juu wa serikali ya China, ni sharti yachunguzwe.

Matangazo ya kibiashara

Peng mwenye umri wa miaka 35, hajaonekana tangu kuonekana kwa barua pepe kwenye mitandao ya kijamii iliyoeleza madai hayo, kuwa alinyanyaswa kimapenzi wiki mbili zilizopita.

Serena amesema ni sharti watu wengine wajitokeze na kulaani kilichotokea huku akisema anatumai kuwa mchezaji huyo wa China atapatikana.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi kuhusu hali ya Peng baada ya kudai kuwa, alilazimishwa kujihusisha kimapenzi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Zhang Gaoli.

Rais wa Shirikisho la mchezo wa Tennis kwa upande wanawake, Steve Simon amesema mchezaji huyo wa China anastahili kusikilizwa na  sio kushtumiwa.