Kocha Ole Gunnar Solskjaer afutwa kazi na klabu ya Manchester United
Imechapishwa:
Klabu ya soka ya Manchester United nchini Uingereza, imemfuta kazi kocha wake Ole Gunnar Solskjaer.
Hii imekuja baada ya klabu hiyo kufungwa na Watford mabao 4-1 katika mechi ya ligi kuu ya soka nchini humo siku ya Jumamosi.
Nafasi yake sasa inachukuliwa kwa muda na mchezaji wa zamani, Michael Carrick aliyewahi kuichezea klabu hiyo kati ya mwaka 2006 na 2018.
Kuondoka kwa Solskjaer raia wa Norway hakujawashangaza mashabiki wa klabu hiyo na wapenzi wa kandanda dunia, kwa sababu ya matokeo mabaya ambayo Manchester United imekuwa ikiyapata.
Manchester United can confirm that Ole Gunnar Solskjaer has left his role as Manager.
— Manchester United (@ManUtd) November 21, 2021
Thank you for everything, Ole ❤️#MUFC
Ameondoka Old Trafford wakati United ikiwa katika nafasi ya saba kwa alama 12. Kati ya mechi saba zilizopita za ligi kuu ya soka nchini humo, imepata ushindi mara moja tu kwa kuifunga Liverpool mabao 5-0.
Solskjaer, mwenye umri wa miaka 48, alimrithi Jose Mourinho kwa kipindi cha mpito Desemba 2018 na baadaye kupewa mkataba wa kudumu mwezi Machi mwaka 2019 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mwezi Julai mwaka huu, alikuwa amesaini mkataba mwingine mpaka 2024.