KOMBE LA DUNIA 2022

Maandalizi ya lala salama kuelekea kombe la dunia mwaka 2022

Uwanja wa Al Bayt nchini Qatar
Uwanja wa Al Bayt nchini Qatar © REUTERS/Kai Pfaffenbach

Ni mwaka mmoja kuelekea fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa fainaili, itakayofanyika nchini Qatar mwaka 2022.

Matangazo ya kibiashara

Itakuwa ni kombe la dunia la 22 kuwahi kufanyika, tangu kuzinduliwa kwake mwaka 1930.

Michuano hiyo itaanza kurindima, tarehe 21 mwezi Novemba mpaka Desemba 18 mwaka 2022.

Timu 32 zitashiriki kwenye michuano hiyo, ikiwemo tano kutoka barani Afrika.

Mataifa ya kwanza kufuzu mapema mwezi Novemba ni Brazil na Argentina kutoka America Kusini.

Huku barani Ulaya mwaka mmoja kabla ya michuano hiyo, mataifa 10 yameshajikatia tiketi ya kufuzu na kufikisha idadi ya mataifa yaliyofuzu mpaka sasa kufikia 13.

Mataifa hayo ni pamoja na  (Argentina, Belgium, Brazil, Croatia, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Qatar (Wenyeji), Serbia, Hispania na Uswizi.

Michuano hiyo itachezwa katika kipindi ambacho kiwango cha joto nchini Qatar kitakuwa kati ya Senti gredi 15 mpaka 24.

Viwanja na miundombinu

Fainali hii itafanyika katika katika viwanja vinane.

Ahmad Bin Ali, Al Bayt, Al Janoub, Al Thumama, Education City, (Ras Abu Aboud) na ule wa Lusail ambao kazi inamalizika.

Mechi ya ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Al Bayt ambao utazinduliwa rasmi mwaka 2022.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi ya Mashariki ya Kati na Kiarabu kuandaa michuano ya kombe la dunia.