Syria

Waandamanaji wauawa katika mji mmoja huko Syria

Baadhi ya waandamanaji wanaoshinikiza kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar Al- Assad.
Baadhi ya waandamanaji wanaoshinikiza kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar Al- Assad. Reuters

Vikosi vya usalama nchini Syria vimewaua waandamanaji 13, katika muendelezo wa maandamano ya kudai mabadiliko ya utawala, ambayo yanazidi kushika kasi wakati huu ambapo viongozi wa upinzani wamemaliza mkutano wao nchini Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa upinzani na wanaharakati ambao walikuwa wanakutana nchini Uturuki wamemaliza mkutano wao na kuja na msimamo wa kumtaka Rais Bashar Al- Assad kuondoka madarakani mara moja.
 

Serikali ya Marekani nayo, imeendelea kuzidisha shinikizo kwa Rais Assad kukubali mabadiliko ya kisiasa au kujiuzulu mara moja, kama alivyoainisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Taifa hilo ,Hillary Clinton.
 

Katika kauli yake, Clinton amesema inasikitisha kuona kiongozi wa taifa hilo, akipuuza wito wa wananchi wake pamoja na Jumuiya ya Kimataifa.
 

Badala ya kukubali na kuachia ngazi, Rais Bashar Al- Assad anaendelea kuua wananchi wake kwa kuamrisha majeshi yake kutumia nguvu nyingi kuwadhibiti wananchi hao, wanaomshinikiza Rais huyo kuondoka madarakani na kufanya mabadiliko ya kweli.