UGIRIKI

Papandreau kuachia wadhifa wake wa uwaziri mkuu

waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou
waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou Reuters

waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreau amekubali kujiuzulu wadhifa wake baada ya kufikia makubaliano katika mazungumzo kati yake na kiongozi wa upinzani juu ya uundwaji wa serikali ya umoja.

Matangazo ya kibiashara

Papandreou na mpinzani wake wa kihafidhina Antonis Samaras wamekutana katika meza ya mazungumzo kujadili kuhusu uundwaji wa serikali ya mseto itakayozishirikisha pande zote mbili.

Kulingana na maafikiano serikali hiyo ya mseto ya Ugiriki haitaongozwa na waziri mkuu wa sasa George Papandreu. Jina la waziri mkuu mpya wa serikali linatarajiwa kutangazwa baadae leo.

Majina ya watu wawili ndio yanachomoza huenda mmoja akachukuwa nafasi hiyo, ikiwa ni kati ya waziri wa fedha wa sasa Evangelos Venizelos na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki Kuu ya Ulaya EU Lucas Papademos.