Je uteuzi wa Dr Kim kama mkuu mpya wa benki ya Dunia umezingatia vigezo?

Sauti 10:01
Jose Ocampo (kushoto), Dr. Jim Kim (katikati) na Ngozi Lweala (kulia) wote hawa ndio waliokuwa wagombea wanafasi ya mkuu mpya wa benki ya Dunia
Jose Ocampo (kushoto), Dr. Jim Kim (katikati) na Ngozi Lweala (kulia) wote hawa ndio waliokuwa wagombea wanafasi ya mkuu mpya wa benki ya Dunia Reuters

Mtangazaji wa makala haya, juma hili ameangazia uteuzi wa mkuu mpya wa benki ya Dunia Dr Jim Yong Kim raia wa Marekani mwenye asili ya Korea, huku wakiachwa wagombea wengine wawili Ngozi Lweala ambaye ni waziri wa fedha wa Nigeria aliyekuwa anapewa nafasi kubwa pamoja na Jose Ocampo aliyekuwa waziri wa Fedha wa Colombia.Leo kwenye Gurudumu la Uchumi tunamwangazi Dr Kim ni nani na atakuwa na mchango gani kwenye ukuaji wa uchumi wa dunia, mgeni wetu ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.