Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Rwanda yaendelea kulaumiwa kwa kusaidia waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC huku kitita kikiwekwa kwa ajili ya kukamatwa kwa viongozi wa Al Shabab

Sauti 20:04
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Rwanda Louise Mushikiwabo anayepinga ushiriki wa nchi yake kuwafadhili waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Rwanda Louise Mushikiwabo anayepinga ushiriki wa nchi yake kuwafadhili waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC

Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu Duniani imeituhumu Rwanda kufadhili waasi wanaopambana na serikali ya DRC, Marekani yatangaza kitita cha dola milioni thelathini kufanikisha kukamatwa kwa Viongozi wa Al Shabab, Ajali ya Ndege ya abiria ya Shirika la Dana yasababisha vifo vya watu mia moja hamsini na tisa, Jumuiya ya Kimataifa yaendelea kushinikiza serikali ya Syria chini ya Rais Bashar Al Assad kukaa kando na operesheni ya kijeshi ya Marekani yafanikisha kifo cha Kiongozi nambari mbili wa Kundi la Al Qaeda Duniani Abu Yahya Al Libi.