Mtangazaji wa gurudumu la uchumi juma hili amezungumzia kuhusu kuendelea kuongezeka kwa deni la taifa nchini Tanzania. Amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi dr Oswald Mashindano ambaye anafafanua dhana hii, karibu usikilize sehemu ya kwanza ya mjadala huu.Ungana na Emmanuel Makundi.........
Vipindi vingine
-
Gurudumu la Uchumi Faida ya mfumo wa malipo ya pamoja barani Afrika Mwezi Januari mwaka 2022, benki kuu pamoja na wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, waliunga mkono mchakato ulioanzishwa na benki ya Afrexim, ambayo ilitengeneza mfumo wa malipo uliolenga kurahisisha ufanyaji wa malipo na manunuzi kati ya nchi na nchi, mtu na mtu na biashara kwa biashara barani Afrika.31/05/2023 09:59
-
Gurudumu la Uchumi Changamoto za kilimo na suluhu endelevu kwa bara Afrika Mkutano wa kimataifa uliowakutanisha wakulima kutoka mataifa ya Afrika, Karibian na Pacific waliokutana nchini Rwanda ambapo walijadiliana kwa pamoja changamoto za kilimo ilizishugulikiwe na kupata suluhu endelevu.30/05/2023 10:04
-
Gurudumu la Uchumi Umuhimu wa bara la Afrika kuwa na mfumo wa pamoja wa kufanya malipo kidijiti Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, malipo ya kidijiti au ya kimtandao yanachangia pakubwa katika kujenga msingi imara wa kufikia maendeleo endelevu, kwanini? Ni kwasababu malipo haya yanapokuwa rahisi, salama, ya wazi na binafsi, yatawezesha ukuaji wa fursa kama nishati, maji na mikopo.Katika kipindi hiki utamsikia, Lucy Nshuti Mbabazi, kutoka taasisi ya umoja wa Mataifa ya muungano wa Better than Cash, Lacina Kone, mkurugenzi wa Smartafrica pamoja na Kwizela Aristide Basebya, mtafiti wa Teknolojia za Mawasiliano ya Umma na Matumizi yake serikalini, akiwa Beijing, China.17/05/2023 10:00
-
Gurudumu la Uchumi SmartAfrica: Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Pili Msikilizaji mataifa mengi ya Afrika, sasa hivi yanafanya juhudi kuhakikisha raia wake wanaunganishwa na huduma ya internet, kama moja ya harakati za kuchochea maendeleo kupitia teknolojia.Lakini kwa wananchi kuunganishwa na huduma hiyo ni jambo moja, changamoto iliyoko sasa hivi kwa nchi nyingi za Afrika ni kukosekana kwa miundombinu sahihi kuwezesha hilo.10/05/2023 10:01
-
Gurudumu la Uchumi Smart Afrika:Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Kwanza Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo, ni moja ya ajenda iliyojadiliwa kwa kina katika mkutano wa juma lililopita nchini Zimbabwe, kuhusu namna bara la Afrika linaweza kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano, TEHAMA, kubadili uchumi wake na kurahisisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi wa bara hilo kama vile afya na kilimo.10/05/2023 10:02