Athari ya vita Sudan Kusini kwa uchumi wake na kanda nzima

Sauti 09:34
Wanajeshi wakilinda eneo la mtambo wa mafuta la Upper Nile nchini Sudan Kusini
Wanajeshi wakilinda eneo la mtambo wa mafuta la Upper Nile nchini Sudan Kusini REUTERS/Andreea Campeanu

Msikilizaji juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi tunaangazia mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini na namna ambavyo machafuko hayo yanaathiri shughuli za kiuchumi kwenye nchi hiyo na kanda nzima.

Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa hivi sasa nchini ya Sudan Kusini imeshuhudia uasi mkubwa na mapigano makali kati ya wanajeshi wa Serikali na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

Vita kubwa imeshuhudiwa hivi sasa kwenye maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta kama kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity State ambako waasi wamedhamiria kuhujumu miundombinu yake.

Mbali na uvamizi wa vituo vya mafuta, waasi hawa wamedaiwa kuua mamia ya watu kwenye eneo la Malakal, Jonglei, Bentiu na maeneo mengine ambako kumeshuhudiwa makabiliano huku mamia ya raia wakiendelea kuyakimbia makazi yao.

Hali hii inasababisha hata uchumi wa nchi hiyo kozorota na kushindwa kusonga mbele kimaendeleo, ndio maana mtangazaji wa makala haya, Emmanuel Makundi amemtafuta mtaalamu wa masuala ya uchumi na diplomasia, Dr Wetengere Kitojo kutazama kwakina machafuko haya hasa kwenye nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati.