Mtangazaji wa makala haya juma hili ameangazia siku ya kimataifa ya wafanyakazi duniani, siku ambayo iliadhimishwa tarehe mosi ya mwezi wa 5, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka.
Kwenye makala haya, mtangazaji amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi, George Gandye, ambapo wamezungumzia masuala mengi likiwemo suala la wafanyakazi kudai nyongeza ya mshahara kila mwaka, swali ni je, madai haya yanatija kwa mwekezaji.
Mbali na kudai nyongeza ya mshahara mtangazaji wa makala hii pia amezungumzia suala la tozo ya kodi kwenye mishahara, tozo ambayo inadaiwa kuwaumiza sana wananchi hasa wafanyakazi waliojariwa kwenye sekta binafsi na zile za umma.
Makala hii pia imegusia suala la taaluma na ujuzi wa wafanyakazi.