Miaka 51 ya Umoja wa Afrika, bara hili liko wapi kimaendeleo
Imechapishwa:
Cheza - 09:48
Juma moja lililopita Umoja wa Afrika AU uliadhimisha miaka 51 toka kuundwa kwa umoja huu, lengo likiwa ni kuziunganisha nchi za Afrika na kuwa kitu kimoja katika kujaribu kufikia malengo ambayo yaliwekwa na waasisi wa uhuru wa mataifa haya.
Licha ya mafanikio ambayo yanaelezwa kupatikana toka kuundwa kwa umoja huu, bado kuna changamoto nyingi ambazo zinalikabili bara hili ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe, kulemaa kwa uchumi wa mataifa na kukosekana kwa maji safi na salama kwa kila mwananchi.
Lakini wakati maadhimisho haya yakifanyika kumekuwa na maswali mengi kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa baa la umasikini barani humo licha ya kuwa na rasilimali nyingi ambazo zingeweza kulikwamua bara hili kiuchumi.
Mtangazaji wa makala hii juma hili amejadiliana na wataalamu wa masuala ya uchumi kutoka Kenya na Tanzania kutathmini ni kwakisai gani bara hili limefanikiwa kiuchumi na biashara.
Wataalamu wetu leo ni Dr Honest Ngowi mhadhiri katika chuo kikuu cha mzumbe tawi la dar es salaam nchini Tanzania na James Shikwati mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Nairobi nchini Kenya.