Gurudumu la Uchumi

Mkutano kati ya IMF na mawaziri wa fedha wa kusini mwa Afrika

Sauti 09:55
Mkuu wa shirika la fedha duniani, Christine Lagarde akiwa na rais wa Msumbiji, Armando Guebuza
Mkuu wa shirika la fedha duniani, Christine Lagarde akiwa na rais wa Msumbiji, Armando Guebuza uneca.org

Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia kumalizika kwa mkutano wa kimataifa uliowakutanisha viongozi wa nchi za Kusini wa Afrika na wale wa shirika la fedha duniani IMF mjini Maputo, Msumbiji. 

Matangazo ya kibiashara

Mtangazaji wa makala hii, amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi na Sera, George Gandye akiwa Dar es Salaam Tanzania na kujadili kwa kina yale ambayo viongozi hawa walikubaliana.

Kwenye mkutano huu uliofanyika juma moja lililopita nchini Msumbiji, viongozi hawa wa Afrika na wale wa IMF walitoka na Azimio la Maputo "Maputo Decleration" azimio ambalo litasaidia kuinua uchumi wa bara hilo.

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde
Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde Reuters

Mfano IMF inasema bara hili linatumia dola za Marekani milioni 93 kila mwaka kwaajili ya kuboresha miundo mbinu yake lakini ni asilimi 2 pekee ya barabara zambazo zinafikika barani humo ukilinganisha na asilimia 82 ya barabara ambazo zinapitika barani Asia.

Masuala ya Rushwa, mikataba feki, biashara haramu ya fedha na matumizi sahihi ya rasilimali zilizoko kwenye bara la Afrika ni mambo ambayo viongozi hawa kwa pamoja walijadili kwa kina na kuazimiana.

Mkurugenzi wa shirika la fedha IMF, Christine Lagarde amewataka viongozi wa Afrika kuwa na matumizi sahihi ya fedha za Umma.