Gurudumu la Uchumi

Vijana na changamoto za kiuchumi, ajira kwenye nchi za maziwa makuu

Sauti 09:29
Maelfu ya vijana waliojitokeza kwenye usaili hivi karibuni nchini Tanzania wanaokadiriwa kufikia elfu 10
Maelfu ya vijana waliojitokeza kwenye usaili hivi karibuni nchini Tanzania wanaokadiriwa kufikia elfu 10 Issa Michuzi Blog

Vijana milioni 75 duniani wanaelezwa kuwa hawana ajira, vijana milioni 279 kwenye nchi za kusini mwa jangwa la Sahara wanaelezwa nao kuwa hawana ajira na hakuna mikakati madhubuti iliyowekwa kwaajili ya kuwatengenezea vijana hawa mazingira ya kujiajiri na kuajiriwa kwenye sekta za umma na sekta binafsi.

Matangazo ya kibiashara

Mtangazaji wa makala hii kwa kutambua mchango wa vijana kwenye uchumi wa mataifa yao na kama nguvu kazi ya nchi, amezungumza na vijana toka kwenye ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa makuu kujadili changamoto ambazo zinawakabilia vijana wa Afrika.

wengi wa vijana wamekuwa wakilala kwa Serikali zao ya kwamba zimekosa mipango muhimu ya kuwawezesha vijana na kuwatengenezea mazingira ya wao kujiajiri, changamoto ya mifumo ya elimu inaonekena kuwa kikwazo katika kufikia malengo yao.