Gurudumu la Uchumi

Mifumo ya Elimu inachangia vijana kumaliza vyuo bila kuwa na ujuzi

Sauti 10:00
Stephan Rebernik/Flick'r/CC

Msikilizaji wa rfikiswahili, nchini Tanzania takriban vijana elfu arobaini humaliza vyuo vikuu kila mwaka na kufanya idadi ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira kuongezeka maradufu kutokana na kukosekana kwa soko la ajira.

Matangazo ya kibiashara

Juma moja lililopita takribani vijana laki moja nchini Kenya waliomaliza vyuo vikuu walijitokeza kufanyiwa usaili kwaajili ya kazi ya kujiunga na jeshi la polisi lajini ni vijana elfu kumi pekee ndio waliokuwa wakihitajika.

Nchini Tanzania Vijana elfu kumi walijitokeza kufanyiwa usaili kwaajili ya kujiunga na jeshi la uhamiaji, lakini nafasi zilizokuwa zinahitajika ni sabini pekee, jambo ambalo linaendelea kutoa picha halisi ya janga la ajira kwa vijana.

Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika mashariki na Jumuiya nyingine za bara hili, zimeendelea na juhudi za ndani na zile za kimataifa katika kuhakikisha wanatengeneza nafasi zaidi za ajira kwa vijana lakini pia kuwajengea uwezo kwa vijana hao kuweza kujiajiri pindi wakimaliza chuo.