PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Uchumi

Palestina: Gaza: sekta ya mafuta matatani

Wanajeshi wa Isaeli karibu na mpaka wa Gaza.
Wanajeshi wa Isaeli karibu na mpaka wa Gaza. REUTERS/Ronen Zvulun

Mapigano katika ukanda wa Gaza yamesababisha hasara ya dola kati ya bilioni 4 na 6, naibu waziri wa uchumi wa Palestina, Tayssir Amro amesema, akibaini kwamba nchi fadhili zinapaswa kukutana mwezi Septemba ujao nchini Norway ili kutathmini hali hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Tayssir amesema hasara hio ni upande wa sekta ya mafuta peke, na iwapo zitajumuishwa sekata zingine huenda hasara ikaongezeka mara dufu.

Naibu waziri huyo amesema Mamlaka ya palestina inapanga kufanya hivi karibuni uchunguzi na ukaguzi ili kujua hasara hiyo imefikia kiwango gani.

Tayssir amebaini kwamba wanasubiri hali ya utulivu irejeye katika ukanda wa Gaza ili waanzishe ukaguzi huo. Watu zaidi ya 1.850 wameuawa na wengine zaidi ya milioni moja wameyahama makaazi yao kufuatia mapigano katika ukanda wa Gaza, baada ya Israeli kijeshi kuvamia eneo hilo, linalokaliwa na watu wengi nchini Palestina.

Tayssir hakutoa taarifa zaidi kuhusu mkutano huo wa wafadhili wa Palestina

Israeli na Hamas ambayo inashikilia mamlaka ya ukanda wa Gaza, wametekeleza tangu mapema jumanne asubuhi makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72, huku jeshi la Israeli likiwa limejiondoa kwenye aridhi ya Gaza kwa siku ya 29 ya mashambulizi ya anga na aridhini.

Nchi ya Palestina inakabiliwa na uhaba wa maji pamoja na matatizo mengine mengi mkiwemo umeme tangu mwaka 2006 Israeli ilipoiwekea vikwazo vya raia wake kutoondoka nje ya nchi.