Gurudumu la Uchumi

Mugabe ataka nchi za SADC kuendeleza viwanda kuimarisha uchumi

Sauti 10:00
Robert Mugabe, rais wa Zimbabwe akizungumza kwenye mkutano wa 34 wa SADC mjini Harare
Robert Mugabe, rais wa Zimbabwe akizungumza kwenye mkutano wa 34 wa SADC mjini Harare REUTERS/Philimon Bulawayo

Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi, mwandaaji wa makala hii ameangazia yale yaliyokubaliwa na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, maazimio ambayo yalifikiwa kwenye mkutano wa mwaka wa jumuiya hiyo mjini Harare Zimbabwe.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mkutano huu, viongozi hawa walikubaliana kuwa mwaka 2014 uwe ni mwaka wa kuboresha viwanda vyao kama njia mojawapo ya kuongeza ushindani na kuhakikisha kwamba mazao yanayozalishwa kwenye nchi wanachama yanatengenezewa barani humo na kuuzwa nje.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo, rais wa Zimbabwe akichukua kijiti cha uongozi toka kwa rais wa Malawi, Peter Mutharika, amewataka viongozi wenzake kuhakikisha wanafufua viwanda vyao na kuvijengea uwezo wa kuwa vinatengeneza malighafi zote kwenye mataifa yao na sio kuziuza na kwenda kutengenezewa nje.