Gurudumu la Uchumi

Wataalamu: China haiwezi kuwa suluhu ya matatizo ya kiuchumi kwenye nchi za Afrika

Sauti 09:44
Aliyekuwa rais wa China Hu Jintao akisalimiana na rais wa Afrika Kusini, Jackob Zuma
Aliyekuwa rais wa China Hu Jintao akisalimiana na rais wa Afrika Kusini, Jackob Zuma Reuters

Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi itaangazia uhusiano uliopo kati ya mataifa ya bara la Afrika na nchi ya China, taifa ambalo kwa kiasi kikubwa limeendelea kuwekeza mabilioni ya dola za Marekani kwenye nchi mbalimbali za Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Wapo wanaoona kuwa ufadhili wa nchi ya China kwa bara la Afrika ndio suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayoyakabili mataifa haya, kwakuwa imekuwa haina maswali mengi kama nchi za Magharibi.

Wapo pia wanaodai kuwa ufadhili wa nchi ya China sio suluhu hata kidogo ya matatizo ya kiuchumi barani Afrika kwakuwa ni mataifa ya Afrika yenyewe yanapaswa kutumia rasilimali ilizonazo kujikwamua kiuchumi kabla ya kukaribisha uwekezaji wa China.

Je ni kweli Afrika inaweza ikawa koloni la Uchina kiuchumi? hili ni moja ya swalia ambalo mtayarishaji wa makala haya anajadili na Dr Honest Ngowi mhadhiri wa masuala ya uchumi toka chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es Salaam nchini Tanzania.