Gurudumu la Uchumi

Wataalamu: Binadamu anahitaji kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha

Sauti 09:48
Reuters/路透社

Mtangazaji wa makala hii juma hili ameangazia ni namna gani mwananchi au wananchi wa kawaida tunautamaduni wa kufanya bajeti ya matumizi ya fedha tunazozipata, ama zitokane na mishahara au biashara.Suala la ubanaji matumizi halihusu Serikali peke yake kwani hata mwananchi wa kawaida usipokuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha unazopata, mwisho wa siku tutaishia kulalamika hela ngumu au gharama ya maisha imepanda.

Matangazo ya kibiashara

Hili ndilo jambo ambalo mtayarishaji wa makala hii amezungumza na wananchi na wataalamu wa saikolojia na uchumi kulidadavua ili kukusaidia wewe mwananchi kuwa na utamaduni wa ubanaji matumizi yako.