Gurudumu la Uchumi

Kwanini IMF inainyima Zimbabwe msaada mwingine wa fedha kunusuru uchumi wake.

Imechapishwa:

Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi tunaangazia kuhusu hatua ya shirika la fedha duniani IMF kutamka wazi kuwa kwasasa haiwezi kuipatia msaada wa fedha nchi ya Zimbabwe mpaka pale nchi hiyo itakapoweza kulipa deni lake.

Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya pili kwa IMF kuikatalia kuipa msaada wa fedha nchi ya Zimbabwe ili ijinusuru kutoka kwenye mdororo wa kiuchumi.

Zimbabwe yenyewe inasema kuwa kwasasa haina uwezo wa kulipa kiasi cha fedha inachodaiwa na IMF na kwamba inaomba isamehewe deni lake lote na kisha ipatiwe mkopo huo ambao inauhitaji wakati huu.