Gurudumu la Uchumi

Nini hatma ya uchumi wa Zambia hata baada ya kifo cha rais Sata

Sauti 09:05
Rais wa Zambia, Marehemu, Michael Sata.
Rais wa Zambia, Marehemu, Michael Sata. REUTERS/Siphiwe Sibeko/Files

Mtangazaji wa makala hii, juma hili anaangazia hatma ya uchumi wa taifa la Zambia hata baada ya kifo cha rais wake, Michael Sata ambaye alifariki Jumatano ya wiki hii wakati akiendelea na matibabu yake jijini London Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Mtangazaji, raia wanaoishi Zambia na wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaangazia kwa kina hali ya uchumi wa nchi ya Zambia wakati wa utawala wa rais Sata, kabla na hata baada ya kifo chake.

Rais Sata wakati wa uhai wake alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa nchi za kusini mwa Afrika aliyeingia madarakani na kuanza kushughulikia mapema zaidi uchumi wa nchi yake pamoja na kupambana na walaji rushwa kwenye taifa hilo harakati ambazo licha ya kuwa alifanikiwa kwa sehemu lakini alianza kukosolewa na wapinzani wake.

Nchi ya Zambia ni nchi inayotegemea sana sekta ya madini na has shaba.